Tuesday, February 25, 2020

Athari za kulala sana kwa mwanadamu


Imebainika kuwa kulala zaidi ya masaa 9 usiku na zaidi ya dakika 90 wakati wa mchana kunaweza kuongeza hatari ya kupigwa na kiharusi.

Matokeo haya yameonyeshwa kwenye jarida la "Neurology" lililochapishwa nchini China baada ya kuwafanyia utafiti watu 31,750 wenye umri wa takriban miaka 62.

Mwanzoni mwa utafiti, iligundulika kuwa wale ambao hawakuwa na tatizo kupooza au shida zingine kubwa za kiafya ni wale wanaolala chini ya masaa nane ukilinganisha na wale ambao hulala masaa tisa.

Hatari ya kupooza imeonekana kuongezeka  kwa asilimia 25 kwa watu ambao walipumzika kwa zaidi ya dakika 90 mchana mara kwa mara, ikilinganishwa na wale ambao walipumzika kwa saa isiyozidi moja au ambao hawakulala usiku.

Utafiti pia umebaini kuwa wale ambao hulala kwa muda mrefu usiku na kulala muda mrefu wakati wa mchana wana uwezekano wa 85% ya kupooza.

Wakati wa utafiti huo, watu walichunguzwa kwa muda wa miaka sita na 1557 kati yao walipooza kwenye harakati za kuchunguzwa.

Hizi hapa sababu za kutumia limao kila siku asubuhi


Tafiti zimebainisha kuwa mtu anashauriwa kutumia maganda ya ndimu kama ambavyo anatumia juisi ya limao kwani maganda hayo yanavirutubisho muhimu sana katika mwili wa binadamu hasa katika kupambana na kiwango cha sukari ndani ya mwili.

Aidha, utumiaji wa juisi ya limao kila siku asubuhi una faida kubwa sana katika mwili wa binadamu, kwani limao ina virutubisho na madini mbalimbali kama Calcium, Magnesiam, vitamin C, Zink, Potasiam, kopa, chuma na Protini.

Hivyo mbali na mwili kurutubika na madini tajwa hapo juu, unywaji wa juisi ya limao, kachumbali ya limao au maji ya vuguvugu yaliyonyunyiziwa limao husaidia mwili katika mambo yafuatayo.

Limao husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kulainisha choo, hivyo kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo la kupata haja kubwa wanashauriwa kila siku asubuhi kutumia juisi ya limao ili kusaidia kupata haja kubwa kwa urahisi.

Limao hutunza mfumo wa kinywa hasa kwa kujali afya ya meno, utumiaji wa limao kila siku asubuhi husaidia kubadilisha rangi ya meno yako hasa wale wenye meno ya njano ndimu husaidia kung’arisha meno nakuyafanya yawe katika hali ya kawaida ya uweupe, hivyo kwa lengo hili inashauriwa uweke vitone vichache katika mswaki wako wakati wa kupiga msawaki ili kupata matokeo hayo kwa urahisi zaidi.

Hutunza nywele, inashauriwa wakati mwingine kuchungua kiasi fulani cha ndimu nakupaka katika nywele hii husaidia kufanya nywele zako kuwa zenye afya na kwa wale wenye nywele chache limao husaidia kujaza nywele na kuzing’arisha na kuzifanya zipate muonekano wa asilia.

Moja ya faida kubwa ya limao ni kupunguza uzito  wa mwili, madaktari wanasisitiza kila asubuhi mtu kutumia glasi ya maji yaliyochanganywa na ndimu pamoja na asali husaidia mfumo wa kuyeyusha mafuta ndani ya mwili na kumfanya mtu apunguze uzito.

Limao husaidia kuepusha kupata uvimbe kwenye figo kwani ndimu inamiliki virutubisho ambavyo huzuia figo kuathirika na uvimbe.

Limao mwilini hufanya kazi ya kuchuja sumu katika ini na figo kutokana na kazi yake ya kusafisha vijidudu vyote vinavyosababisha bacteria wabaya mwilini.

Limao inaongeza kinga mwilini ya kupigana na magonjwa mbalimbali, na ndio maana inashauriwa kwa wale wenye kinga pungufu dhidi ya magonjwa kutumia limao ili kuipa nguvu kinga ya mwili kupingana na magonjwa mbalimbali.

Maajabu yatokanayo na mkungu kiafya


Mkungu ni mti unaoweza kuota porini au wengine huupanda kwenye makazi wanayoishi. Kwa wanaoupanda nyumbani, moja ya faida wanayoipata ni kivuli chenye ubaridi asilia.

Mti huu wenye majani mapana kiasi, unazaa matunda maarufu kama kungu. Watu wazima hususani kinamama na watoto wanapenda kuyala matunda hayo.

Pamoja na kuzoea kuyala, bado wengi miongoni mwao hawafahamu faida zake. Wanakula kwa kusukumwa zaidi na mazoea. Kama nilivyosema awali asili yake ni mti pori una faida nyingi kitiba kuanzia majani hadi mizizi.

Hata hivyo, baadhi ya watu wanaamini kuwa mti huu unapokuwa umepandwa au kuota wenyewe jirani au kwenye makazi ya watu, unahusianishwa na imani za kishirikina kuwa ni makazi ya pepo wabaya, dhana ambayo ni potofu. Mti huo ni kama miti mingine ya kivuli na matunda.

Kama nilivyosema hapo awali kungu zina faida nyingi ikiwamo kusaidia mmeng’enyo wa chakula kufanyika ipasavyo tumboni kwa kuwa zimesheheni wingi wa vitamini B6, B12 na C na zina utajiri wa madini ya zinki.

Majani ya mkungu yakikaushwa kivulini na kutwangwa, unga wake ukitumiwa katika uji usio mzito au maji moto unasaidia kuondoa homa mwilini, tatizo la taifodi na ini.

Pia unasaidia tatizo la vidonda vya tumbo na uzazi kwa kinamama, maumivu ya hedhi na mwasho sehemu za uzazi na hivyo kumfanya mama abaki katika hali ya furaha.

Zijue athari za kuvaa viatu virefu wakati wa ujauzito


Kipindi cha ujauzito ni wakati wa kubadili mambo mengi katika mfumo wa maisha wa mjamzito. Moja ya mambo makubwa ni pamoja na tabia ya kuvaa viatu vyenye visigino virefu. Mjamzito hashauriwi kuvaa viatu vyenye visigino virefu kutokana na athari zinazoweza kutokana na aina hizi za viatu.

Zifuatazo ni athari za kuvaa viatu vyenye visigino virefu wakati wa ujauzito:


Maumivu ya misuli ya mapaja.
Wadada hupenda kuvaa “high heels” husababisha misuli ya mapaja kukaza na kuwa na muonekano mzuri. Katika ujauzito, mabadiliko ya homoni huweza kupelekea misuli hii kuwa na maumivu tofauti na ilivyokua kabla ya ujauzito.

Maumivu ya mgongo.
Wakati wa ujauzito, uzito mkubwa huhamia mbele na misuli ya nyonga hulegea. Mabadiliko haya ya kimsawazo huweza kusababisha maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo na kiuno.

Hatari ya kuanguka.
Ni wazi kuwa uzito huongezeka wakati wa ujauzito na mabadiliko ya vichocheo vya mwili huweza kupelekea kizunguzungu cha hapa na pale. Hii huongeza hatari ya kuanguka iwapo utavaa “high heels” na kupelekea majeraha kwako na kwa mtoto aliyeko tumboni.

Uvimbe miguuni.
Ni jambo la kawaida miguu kuvimba wakati wa ujauzito. Kuvaa viatu vyenye visigino virefu na vyenye kubana huweza kuongeza tatizo hilo na kupelekea maumivu.

Mimba kutoka.
Mjamzito akivaa viatu vyenye visigino virefu anakua katika hatari kubwa ya kuanguka. Hii huweza kusababisha majeraha makubwa kwa mtoto aliyeko tumboni hali inayoweza kusababisha mimba kutoka.

Lakini, iwapo kuna ulazima sana wa kuvaa viatu hivyo, unapaswa kuzingatia yafuatayo:
Ni salama kuvaa viatu hivi katika muhula wa kwanza wa ujauzito (Miezi mitatu ya mwanzo).
Viatu visiwe virefu sana na visigino viwe imara.
Vaa viatu visivyo na bugdha na usivikaze sana.
Epuka visigino vyembamba sana.
Usivae siku nzima. Vitoe mara kwa mara kupumzisha miguu.
Epuka kutembea au kusimama muda mrefu ukiwa umevivaa.
Ukihisi maumivu kwenye misuli ya mapaja jaribu kufanya mazoezi ya kujinyoosha na kujikanda.

Kiasi cha maji unachopaswa kunywa kulingana na uzito wako


Ni kiasi gani cha maji unakunywa kwa siku na unakunywa wakati gan!

Kama tunavyojua kuwa maji ni uhai, maji yakinywewa kwa nidhamu na kuzingatia uzito mtu alionao tunaweza kukwepa zaidi ya asilimia sitini (60%) ya maradhi mbalimbali.


Muda gani sahihi wa kunywa maji!
Mara tu unapoamka asubuhi.
Nusu saa au dk 45 kabla ya muda wa chakula  cha mchana au cha jioni.
Na muda uliobaki kunywa kiasi kwa kipindi fulani cha muda.
Yanywe maji ukiwa umekaa na kunywa kidogo kidogo.

Muda gani usinywe maji!
Usinywe maji wakati au mara tu baada ya kula. Ijulikane kuwa maji na chakula ni vitu viwili tofauti ambavyo mwili unahitaji lakini sio kwa mkupuo. Ukifanya hivyo maji yanaharibu baadhi ya virutubisho vilivyopo kwenye chakula.
Usinywe maji mengi kwa wakati mmoja ili kufikia kiwango kinachohitajika kwa siku.
Hakikisha inapofika saa 12 jioni uwe umeshafikia kiwango chako cha mwisho, usinywe maji zaidi ya muda huo yatakuharibia usingizi usiku.

Kiasi gani cha maji ninywe kwa siku kulingana na uzito nilionao!
Angalia kwenye picha iliyoambatanishwa chini ya makala hii upate kujua kiasi unachotakiwa kunywa kulingana na uzito ulionao.