Monday, March 23, 2020

Siri za kuishi miaka mingi zaidi

Kuishi karne moja au zaidi duniani ni mafanikio makubwa katika maisha ya binadamu lakini kutokana na kuongezeka sababu zinazopelekea mtu kufa mapema ikiwemo hali ngumu ya maisha na kukosa furaha na amani, imeelezwa kuwa ili uishi muda mrefu ni lazima ufanikiwe katika afya.

Wapo watu waliowahi kuishi miaka 100 na zaidi na wengine wapo hata sasa huku wengi wakiwa na siri za kuishi muda mrefu kiasi hicho.

Mtandao wa indiatime.com kwa msaada wa watu walioishi kwa miaka mingi duniani umezitaja siri 7 ambazo zikizingatiwa zinaweza kumfanya mtu akaishi kwa muda mrefu zaidi.

Kutembea sana kwa miguu
George Boggess hakufikisha miaka 105 lakini aliishi zaidi ya miaka 100 aliwahi kutoa ushauri na siri ya kuishi umri mrefu kuwa ni kutembea.

Kula samaki na kulala kwa angalau saa 8
Misao Okawa, ambaye alitambulika kama binadamu mkwenye umri mkubwa zaidi dunia ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 117 alisema sushi (samaki) na saa 8 za kulala ni siri ya kuishi kwa muda mrefu.

Wajapan wanatajwa kuwa na uwiano wa kuishi muda mrefu mbapo kuna zaidi ya watu 5,000 wanaosemwa kuishi zaidi ya mika 100.

Kupiga push-ups tano hadi saba kila siku
Duranord Veillalord ambaye alitimiza miaka 109 mwaka jana anaianza siku yake kwa pushups kila siku. Pushups, kikombe cha chai na matunda ni siri ya kuishi kwa miaka mingi.

Kaa mbali na vipodozi
Adelina Domingues alikuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuishi Marekani ambapo alifariki akiwa na umri wa miaka 114 anasema siri kubwa ya yeye kuishi miaka mingi ni kujiweka mbali na vipodozi.

Kunywa uji wakati wa kufungua kinywa
Jesse Gallan aliishi kwa miaka 109 na kusema siri kubwa ilikuwa kunywa uji kama kifungua kinywa chake pia alisema kutokuwa na wanaume wengi kwenye maisha yake kuliongeza miaka ya maisha yake.

Kaa mbali na pombe/ulevi
Alexander Imich wa New York City ambaye aliishi kwa miaka 111 alisema siri kubwa ya yeye kuishi miaka 111 ni kwa sababu alijiweka mbali na kilevi na alikuwa muogeleaji na kufanya mazoezi. Chakula chake kilikuwa ni kuku na samaki na kuishi maisha ya kuzingatia kanuni za kiafya.

Kula kwa kiasi


Wanawake wa jamii ya Hunza inayopatikana katika mipaka ya Kashmir, China na Afghanistan hupata watoto wakiwa na miaka 60 na wanaume wanaoonekana kama wana miaka 40. Wazee wa jamii hii wamefikisha umri wa miaka mia moja na wangali na muonekano kana kwamba wana miaka 70 ambapo wanajamii hiyo wakisema siri ni kula kwa kiasi. Wanakula nyama kidogo katika milo miwili kwa siku.

Mbinu za asili za kuongeza nguvu za kiume


Upungufu wa nguvu za kiume umekua tatizo kubwa sana kwa wanaume wengi. Tatizo hili limewakumba wanaume wengi walio katika ndoa na hata wale ambao bado hawajaoa.

Watu wengi wamekuwa wakisumbuka kutafuta utatuzi kwani tatizo hili huwafanya kuwa na wasiwasi wa maisha. Ndoa nyingi zimevunjika na mahusiano kuharibika kwa sababu ya tatizo hili.

Kwa wanaume wenye umri mkubwa, upungufu wa nguvu za kiume unaweza usiwe ni tatizo kwani miili yao inakuwa tayari imechoka.

Hizi hapa ni baadhi ya njia zitakazokusaidia kurudisha nguvu za kiume zilizokuwa zimepotea, au kuimarisha uwezo wako wa tendo la ndoa.

Jitahidi kutumia vinywaji na vyakula visivyokuwa na sukari nyingi.
Epuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi kwani ni adui mkubwa sana wa afya yako hasa wakati unataka kurudisha nguvu za kiume. Kula vyakula asili na nafaka ambayo haijakobolewa, kula matunda kwa wingi pamoja na mboga za majani. Utafurahia maisha ya kula vyakula asili na utakuwa imara katika tendo la ndoa.

Epuka unywaji wa Pombe.
Tafiti zinaonesha kwamba pombe inakupa hamu au shauku ya kufanya tendo la ndoa lakini inakunyima uwezo wa kufanya tendo hilo, kwani hupunguza kiwango cha maji mwilini.

Fanya mazoezi ya viungo.
Watu wengi wameelemewa na magonjwa kwa sababu tu mwili haupatishi damu ya kutosha kwenda sehemu mbali mbali kama vile ubongo, ini na figo ambazo ndio sehemu zenye kuufanya mwili wako ufanye kazi katika uhalisia wake. Uume ili usimame kwa uimara, unatakiwa upate damu ya kutosha.

Kufanya mazoezi hupunguza kiwango cha mafuta katika mishipa ya damu na kuiwezesha kupeleka damu ya kutosha katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo uume.

Rudisha virutubisho ambavyo vimepotea mwilini mwako.
Hakikisha mwili wako unaupa madini ya msingi kama zinki, chuma, selenium, manganese na vitamin nyingi, kwani madini haya ndiyo yanafanya mwili wako ufanye kazi katika kiwango stahiki. Madni haya huwezesha viendesha shughuli za mwili yani enzymes kufanya kazi katika kiwango kizuri na kuimarisha mwili wako. Madini haya hupatikana katika mboga, samaki na matunda ya aina mbalimbali.

Kunywa maji ya kutosha kila siku.
Kunywa maji ya kutosha kila siku, usingoje mpaka kiu ikupate. Mtu mzima anapaswa kunywa maji glass 8 mpaka 10 kwa siku. Maji husaidia kuongeza kiwango cha damu na kuondoa sumu mbalimbali mwilini.

Epukana na msongo wa mawazo.


Ufanyaji wa tendo la ndoa huwa unahusisha mambo mengi. Unaweza ukawa umekamilika kiafya lakini ukashindwa kufanya mapenzi kwa kuwa una msongo wa mawazo. Hakikisha kabla ya kwenda faragha na mpenzi wako, unauituliza akili na usiwaze mambo mengine nje ya tendo linaloenda kufanyika. Hii itakupa muda mzuri wa ubongo wako kupeleka damu ya kutosha katika uume.

Umuhimu wa afya ya akili

Afya yako ya akili inahusiana na jinsi unavyojihisi na akili yako inavyofanya kazi. Afya yako ya akili ni muhimu sana kwa sababu inaweza kuathiri afya yako ya kimwili na ustawi wako wote.
           
Wakati mtu ana shida ya afya ya akili, inamaanisha ustawi wao wa akili hauko sawa kama vile mwili wako unapoumia. Kuna sababu nyingi ambazo watu hupata masuala ya afya ya akili.

Wanaume wengine huzaliwa katika hatari kubwa zaidi na wengine wana hatari baada ya kukabiliana na mambo kama msongo wa mawazo au shida.

Wakati mwingine matatizo ya afya ya akili yanaweza kuwa madogo na kuisha kwa urahisi. Nyakati nyingine yanaweza kuwa mabaya na kufanya iwe vigumu kwa watu kufanya kazi kama kawaida.

Wanaume wanaojamiiana na wanaume wengine wanaweza kupata matatizo ya afya ya akili kama huzuni na wasiwasi, sio kwa sababu ya wale wanaojamiiana nao lakini kwa sababu wanaweza kupata unyanyasaji, unyanyapaa, na ubaguzi.

Kuwa na uwezo wa kutambua ugonjwa wa akili ni muhimu kwa sababu wakati mwingine unaweza kukuongezea hatari ya kupata VVU kwa kuongeza matumizi ya vilevi au ya ngono hatari.

Jinsi ya kujikinga na vidonda vya tumbo

Nini husababisha vidonda vya tumbo?
Kisababishi kikuu ni bakteria aina ya helicobacter pylori ni kupitia vyakula na maji. Pia, hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo kama wapenzi wanaonyonyana ndimi.

Bakteria hao huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng’enya viitwayo urease inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.

Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.

Sababu nyingine ni chembe za urithi genetics. Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu na wenye vidonda pia. Hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.

Uvutaji sigara na tumbaku. Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta. Matumizi ya pombe/vilevi. Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo.

Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.

Dalili za vidonda
Ieleweke ni mara chache mtu kuugua vidonda vya tumbo na kutoonyesha dalili.

Zifuatazo ni dalili zinazotokea kwa wagojwa wengi;
Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda.
Maumivu yanaweza kuanzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua.
Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia, yanaweza kuwa makali wakati wa usiku yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo.


Dalili nyingine ni kushindwa kumeza vizuri chakula au kukwama kama kinataka kurudi mdomoni, kujisikia vibaya baada ya kula, kupungua uzito, kukosa hamu ya kula.

Dalili hatari ni pamoja na kutapika damu, kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito na kupata kichefuchefu na kutapika.

Jinsi ya kugundua vidonda vya tumbo
Maelezo ya mgonjwa kuhusu dalili humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mgonjwa kuwa ni vidonda vya tumbo.

Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika. Kupima damu kuangalia bakteria aina ya h.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors ‘PPIs’ mfano Omeprazole. Vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi.

Kupima pumzi. Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya saa moja mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa. Ikiwa mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.

Kupima antijeni kwenye kinyesi. Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria h.pylori kwenye kinyesi. Vilevile kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria.

Kufanya x-ray ya sehemu ya juu ya tumbo ‘upper gastrointestinal x-ray’. Picha huonyesha ‘esophagus’, mfuko wa tumbo ‘stomach’ na dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye ‘Barium’ ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwenye x-ray.

Matibabu
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria h.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na ‘NSAIDs’ na hana maambukizi ya bakteria h.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors ‘PPIs’ mfano Omeprazole, Esomeprazole & Lansoprazole.

Proton Pump Inhibitors ‘PPIs’ hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo ‘Proton Pump’ ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni.

Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatarithiwa na dawa kama Paracetamol.

Vilevile dawa aina ya H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine, hutumika kama mbadala kama dawa aina ya ‘PPIs’ hazitokuwepo.

H2-Receptor Antagonists hufanya kazi ya kuzuiia utendaji wa protini iitwayo ‘Histamine’ ambayo inahusika na kuchochea utengenezaji wa asidi tumboni.

Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi, hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi ‘Antiacids’ & ‘Alginates’ kwa ajili ya nafuu ya haraka.

Namna ya kuishi na vidonda vya tumbo
Mambo yafuatayo yatakusaidia kuishi vizuri ukiwa na vidonda vya tumbo;kuacha kutumia kahawa na chai, kwani vitu hivi huongeza kiwango cha asidi kinachotengenezwa na tumbo lako. Unaweza kutumia chai ya mitishamba kama mbadala.

Kunywa maziwa na vitu vitokanavyo na maziwa kama maziwa mgando na jibini.

Maziwa hufikiriwa kufunika utumbo na kupunguza athari za asidi ya tumboni. Jitahidi kupunguza uzito hasa ikiwa uzito umezidi na hauendani na kimo chako.

Kula angalau kidogo mara kwa mara. Hii itasaidia kupunguza athari za asidi inayotengenezwa na tumbo.

Acha au kunywa vileo siku maalumu tu kwa maana unywaji wa pombe mara kwa mara hutonesha kwenye vidonda vya tumbo vinavyotaka kupona.

Epuka matumizi ya viungo vya vyakula kwa maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi.


Acha kuvuta sigara, tumbaku, na bangi. Uvutaji wa sigara utakuweka kwenye hatari zaidi ya kuanza vidonda vipya na kuzuia vidonda vingine visipone.

Monday, March 16, 2020

FAIDA ZA LIMAO AU NDIMU KILISHE NA AFYA


Zifuatazo ndizo faida zitokanazo na utumiaji wa limao na ndimu kilishe na kiafya;
Kusaidia uwiano sahihi wa pH ya mwili kuuwezesha kufanya shughuli mbalimbali.

Ina vitamin C na kemikali mimea ambayo husaidia kutibu mafua na mfumo wa upumuaji. Pia kuboresha afya ya ngozi, fizi (kuzuia fizi kutoka damu, ukavu wa ngozi ikiwemo kuchanika midomi na pua kavu), moyo, figo, misuli, maini na ubongo kwa kupambana na sumu mbalimbali mwilini. Pia husaidia kukata uchovu wa mazoezi au marathon.

Husaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, kunywa sharubati yenye mchanganyiko wa limao au ndimu, au bilauli ya maji ya limao au ndimu nusu saa kabla ya kula.

Pia tindikali zilizonazo husaidia kuzuia au kupambana na vijiwe vya figo, gout (mlundiknoi wa uric acid kwenye viungo na mwili). Husaidia kufyonzwa na kubadilisha madini ya chuma kwenye vyakula jamii ya mimea na kufanya iweze kutumika kutengeneza damu (ferrous iron).

Ganda la limao pia lina virutubisho, kemikali mimea na mafuta kwa wingi. Ganda lake au mafuta husaidia kutibu mafua, kuchua misuli au hutumika kwenye vinywaji kuleta ladha au kama tiba mvuke kwa magonjwa ya msongo wa mawazo, au magonjwa ya mifumo ya fahamu.

Matumizi ya mara kwa mara Husaidia kupambana na kisukari, shinikizo la damu (kutokana na wingi wa potassium) na ulemavu wa macho.

Matumizi ya kila siku kwa muda mrefu Husaidia kuzuia saratani mbalimbali mwilini.
Husaidia mchakato wa kuzalisha nguvu mwilini.

 Mambo muhimu ya kuzingatia.
Inashauriwa kuongeza limao/ndimu kwenye mboga za majani kama tembele na chai ili kusaidia ufyonzwaji na utumiwaji wa madini ya chuma mwilini toka kwenye mboga hizo.

Faida hizi pia zafanana na jamii zote za malimao yakiwemo machungwa, madalansi, machenza nk japo baadhi ya faida zinaweza kuwa kwa wingi au kidogo kwa kila tunda

Inashauriwa kutumia moja ya matunda hayo kila siku ili kuboresha lishe na afya zetu.

Angalizo
Wapo wanaotumia limao kuondoa kichefuchefu au kuzuia kutapika, ila limao halizuii kutapika, bali inapelekea kutapika kutokana na uchachu wake. Hivyo waweza tumia parachichi au tunda baridi (lisilo chachu) kuzuia kutapika

TAMBUA DALILI NA NAMNA YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA


Corona ni ugonjwa wa homa kali ya mapafu inasababishwa na virusi vya Corona ni ugonjwa unaoambukizwa kwa kuingiwa na majimaji yatokanayo kwenye njia ya hewa wakati mtu mwenye ugonjwa huu anapokohoa au kupiga chafya.







Sunday, March 15, 2020

TAMBUA DALILI NA NAMNA YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA COVID-19


Corona ni ugonjwa wa homa kali ya mapafu inasababishwa na virusi vya Corona ni ugonjwa unaoambukizwa kwa kuingiwa na majimaji yatokanayo kwenye njia ya hewa wakati mtu mwenye ugonjwa huu anapokohoa au kupiga chafya.