Kifafa ni ugonjwa wa ubongo unaomfanya mtu azimie. Huenda mtu akazimia kwa dakika tano au zaidi ya hapo, lakini watafiti wanasema mtu huzimia kunapokuwa na utendaji usio wa kawaida katika chembe za ubongo.
Sasa kama hali hiyo itajitokeza, hutakiwi kushtuka, tulia na kwa haraka utafute namna ya kumsaidia mgonjwa ili kuokoa maisha yake.
Tovuti ya The Beehive inaorodhesha mambo unayopaswa kufanya kumsaidia mtu mwenye kifafa anapopatwa na ugonjwa huo.
Namna ya kumsaidia mgonjwa wa kifafa
Hatua ya kwanza mzuie taratibu, usijaribu kumzuia kwa kutumia nguvu kama kumshika mikono na miguu kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha majeraha kwa mgonjwa na pia kwa yule anayejaribu kumsaidia.
Ondoa vitu vyote vyenye ncha kali vinavyoweza kumdhuru mgonjwa.
Fungua nguo au kitu chochote kilichopo kwenye shingo ambacho kinaweza kuathiri upumuaji.
Endapo mgonjwa atazimia, weka kitu laini katika kichwa chake na umsaidie alale upande.
Usimpulizie hewa mdomoni, fanya hivyo iwapo hataweza kupumua baada ya kifafa kutulia.
Mgonjwa anapotulia na kurudiwa na fahamu zake muoneshe upendo asihisi kama ametokewa na kitu chochote kibaya.
Ikiwa mgonjwa amezimia kwa zaidi ya dakika 10 hakikisha unamuwahisha hospitali ili kuokoa maisha yake
No comments:
Post a Comment