Wednesday, March 11, 2020

Zifahamu Kanuni za Kulinda Afya ya Figo zako

SIKU YA AFYA YA FIGO DUNIANI

Figo ni ogani muhimu katika uhai hasa kusafisha damu, uimara wa mifupa, kudhibiti presha

KANUNI MUHIMU KULINDA AFYA YA FIGO
1️⃣Zingatia unywaji wa maji
2️⃣Zingatia lishe bora
3️⃣Mazoezi
4️⃣Dhibiti uzito/unene
5️⃣Dhibiti kiwango cha Shinikizo lako la damu
6️⃣Dhibiti kiwango cha sukari kwenye damu
7️⃣Usipende chumvi nyingi
8️⃣Punguza vyakula vya viwandani

Sababu za kiafya za kutumia limao kila siku asubuhi

Tafiti zimebainisha kuwa mtu anashauriwa kutumia maganda ya ndimu kama ambavyo anatumia juisi ya limao kwani maganda hayo yanavirutubisho muhimu sana katika mwili wa binadamu hasa katika kupambana na kiwango cha sukari ndani ya mwili.

Aidha, utumiaji wa juisi ya limao kila siku asubuhi una faida kubwa sana katika mwili wa binadamu, kwani limao ina virutubisho na madini mbalimbali kama Calcium, Magnesiam, vitamin C, Zink, Potasiam, kopa, chuma na Protini.

Hivyo mbali na mwili kurutubika na madini tajwa hapo juu, unywaji wa juisi ya limao, kachumbali ya limao au maji ya vuguvugu yaliyonyunyiziwa limao husaidia mwili katika mambo yafuatayo.

Limao husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kulainisha choo, hivyo kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo la kupata haja kubwa wanashauriwa kila siku asubuhi kutumia juisi ya limao ili kusaidia kupata haja kubwa kwa urahisi.

Limao hutunza mfumo wa kinywa hasa kwa kujali afya ya meno, utumiaji wa limao kila siku asubuhi husaidia kubadilisha rangi ya meno yako hasa wale wenye meno ya njano ndimu husaidia kung’arisha meno nakuyafanya yawe katika hali ya kawaida ya uweupe, hivyo kwa lengo hili inashauriwa uweke vitone vichache katika mswaki wako wakati wa kupiga msawaki ili kupata matokeo hayo kwa urahisi zaidi.

Hutunza nywele, inashauriwa wakati mwingine kuchungua kiasi fulani cha ndimu nakupaka katika nywele hii husaidia kufanya nywele zako kuwa zenye afya na kwa wale wenye nywele chache limao husaidia kujaza nywele na kuzing’arisha na kuzifanya zipate muonekano wa asilia.

Moja ya faida kubwa ya limao ni kupunguza uzito  wa mwili, madaktari wanasisitiza kila asubuhi mtu kutumia glasi ya maji yaliyochanganywa na ndimu pamoja na asali husaidia mfumo wa kuyeyusha mafuta ndani ya mwili na kumfanya mtu apunguze uzito.

Limao husaidia kuepusha kupata uvimbe kwenye figo kwani ndimu inamiliki virutubisho ambavyo huzuia figo kuathirika na uvimbe.

Limao mwilini hufanya kazi ya kuchuja sumu katika ini na figo kutokana na kazi yake ya kusafisha vijidudu vyote vinavyosababisha bacteria wabaya mwilini.

Limao inaongeza kinga mwilini ya kupigana na magonjwa mbalimbali, na ndio maana inashauriwa kwa wale wenye kinga pungufu dhidi ya magonjwa kutumia limao ili kuipa nguvu kinga ya mwili kupingana na magonjwa mbalimbali

Tuesday, March 10, 2020

BAADA ya Muda Gani Unaruhusiwa Kufanya Mapenzi na Mkeo Baada ya Kujifungua?

Zoezi la kujifungua linafariji na kuchosha pia, ni la faraja sana kwa kuwa linakufanya uwe mama? Wiki 4 za mwanzo kwa mzazi zinaweza kuwa katika kumbukumbu zako kwa muda mrefu kwakuwa ni wiki za ‘majimaji’ tu – jasho, kunyonyesha na haja ndogo kutoa majimaji yote ya ziada mwilini mwako. Inashangaza hata kama mtu utakuwa na hamu ya kufanya mapenzi katika kipindi hicho.

Madaktari wanasema kuwa mwili wa mwanamke unahitaji wiki 6 kurudi kwenye hali yake ya kawaida. Katika kipindi hiki cha wiki 6, mfupa wa nyonga na uti wa mgongo hurudi kwenye hali yake ya awali. Homoni zako pia zinajirekebisha sambamba na misuli iliyopo kwenye sakafu ya nyonga kupumzika wakati ikirudi kwenye hali yake iliyokuwa nayo mwanzo kabla ya kazi kubwa iliyotoka kuifanya ya kumbeba mtoto na kusaidia kwenye kumtoa wakati wa kujifungua.

Kwahiyo, mpaka kitakapofika kipindi hiki cha wiki 6, unashauriwa kutofanya mapenzi, lakini haimaanishi kwamba huwezi kufanya mambo mengine kama kumbusu, kumshikashika, au kumnyonya mwanaume wako, na yeye kukufanyia hivyo hivyo. Wanawake wengine wanasema kuwa chuchu zao huwa na hisia sana kutokana na kunyonyesha kiasi kwamba wanaweza kufika kileleni kwa kushikwa chuchu tu.

Lakini kuhusu dawa za kuzuia kubeba mimba katika kipindi hiki, mnashauriwa muwe na tahadhari kuhusu kutumia njia yoyote itayoathiri mfumo wa homoni. Hii ni kwa sababu itaathiri sana kiwango na ubora wa maziwa na itamsababishia mtoto kutopata lishe inayotakiwa. Pia, vidonge vyenye oestrogen vimethibitishwa kusababisha kupungua kwa kiwango cha maziwa kwa mama anayenyonyesha, na mara nyingine hupunguza ghafla sana.

Shirika la Afya Duniani linasisitiza mtoto anywe maziwa tu kwa muda usiopungua miezi 6 kisha uendelee kumnyonyesha mpaka atakapofikisha miaka miwili. Wazazi wengi wanaona hii inawatesa na wengi wao wanasema kwamba miezi 6 ya mwanzo ni muhimu sana.

Unashauriwa uzungumze na daktari wako kuhusu muda gani unaweza kurudia kufanya mapenzi na njia za kutumia kujikinga na mimba ya haraka na pia umuulize hasa kuhusu kutumia dawa zenye progesterone na madhara yake kwako. Vidonge hivi vinaathiri maziwa (kwa wingi na ubora) kwa kiwango kidogo zaidi ukilinganisha na vidonge vyenye oestrogen.

Mwili wako umefanya kazi kubwa sana ya kuleta kiumbe duniani. Sio tu kwa sababu ni utambulisho wako na kukufanya uitwe ‘mama’ na chochote utachofanya kitakachokufurahisha, utashangaa jinsi ulivyo na sehemu nyingi zinazoweza kukufanya upate raha.

Fahamu kuhusu ugonjwa wa Polio kiundani zaidi

Polio ni ugonjwa wa kuambukiza usababishwao na virusi, huathiri neva na kusababisha ulemavu.

Kutokana na taarifa za shirika la afya duniani:
Polio huathiri zaidi watoto wa umri wa chini ya miaka mitano
Ulemavu hutokea kwa mmoja kati ya maambukizi 200
Mpaka 2013 ni nchi tatu ambazo bado kuna mlipuko wa ugonjwa huu wa kupooza Afghanistan, Pakistan na Nigeria. Ila kutokana na Taarifa kutoka wizara ya afya ya Tanzania ilipokea taarifa kutoka shirika la afya duniani kuwa kuna mlipuko katika nji jirani ya Kenya, wilaya ya Fafi.

Je ni zipi dalili za ugonjwa huu?
Dalili hizi hudumu kwa kati ya siku 1 hadi 10
Homa
Maumivu ya kichwa
Kutapika
Uchovu
Maumivu ya shingo
Maumivu ya mgongo
Maumivu ya mikono na miguu
Misuli kukakamaa

Je ni matatizo gani mtu huweza kupata baada ya maambukizi haya?
Kupooza misuli
Ulemavu wa miguu

Vipimo:
Virusi vya polio huweza kuonekana katika makohozi, kinyesi na maji maji ya uti wa mgongo.

Matibabu
Hamna matibabu ya maambukizi haya, kwahiyo ni tiba ya dalili ambayo hutolewa:
Kupumzika
Dawa za kutuliza maumivu na kushusha homa
Antibiotiki kuzuia maambukizi nyemelezi
Mazoezi kiasi kwaajili ya kuzuia kukakamaa
Na kula chakula bora

Kinga
Ni chanjo ya Polio ambayo hutolewa pamoja na chanjo nyingine kwa watoto baada tu ya kuzaliwa, na kurudiwa tena katika wiki ya nne, ya nane na mwisho ya kumi na mbili.

Monday, March 9, 2020

Faida ya Embe bichi kiafya

Unaweza usiamini nikikuambia embe bichi ni tiba ya ugonjwa furani, lakini amini kuwa kweli ni tiba, tena iliyo makini. Embe bichi linasaidia sana kwa mgonjwa wa maradhi ya kuhara. Tumia embe bichi kumaliza tatizo hilo.

Menya embe bichi, likate  vipande na kuviweka katika chombo, au tengeneza juice changanya na unga wa pilipili manga pamoja na asali, kisha tafuna vipande hivyo vyenye mchanganyiko huo.

Mchanganyiko wako utategemea kiwango cha vipande vya embe lako. Hata hivyo, usile zaidi ya embe mbili kwa kutwa moja. Endelea na tiba hii muda wa siku tatu.

Kuharisha ni kitendo cha kujisaidia kinyesi chenye majimaji mara kwa mara. Hali hiyo hutokea baada ya utumbo mdogo kuwa na maji mengi ambayo yanashindwa kutoka mwiilini kwa njia za kawaida kama ya mkojo na jasho hivyo yanatelemka kwenye utumbo mkubwa usio na uwezo wa kutunza maji.

Yakiwa huko mtu hujikuta anajisikia hali ya kutoa haja na ndipo maji hayo hutoka kupitia haja kubwa. Kimsingi utumbo mdogo una uwezo wa kupokea zaidi ya lita nane za maji kutoka kwenye vyakula au vinywaji vinavyopitia mdomoni na mengine kutoka sehemu mbalimbali katika mwili.

Tatizo la kuhara linaweza kusababishwa na kula kupita kiasi, kula mchanganyiko wa vyakula vya aina mbalimbali, kuwa na hofu, hasira au wasiwasi, kuchacha chakula ndani ya tumbo, kula sumu, bakteria, virusi au vijidudu wenye vimelea.

Sunday, March 8, 2020

Mambo 5 ya kufanya ili kuharakisha kupona Majeraha

Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia.

Kwa kutambua hili karibu nikufahamishe mambo matano unayoweza kuyafanya ili kuharakisha kupona majeraha.

1. Kula vizuri
Lishe bora ni muhimu wakati wote, lakini ni muhimu zaidi mara unapokuwa na majeraha. Ili uweze kupona majeraha mapema unahitaji ule matunda na vyakula vyenye protini, vitamini C, B12 pamoja na madini ya chuma kwa wingi.

Vyakula na matunda hayo ni kama vile machungwa, mapapai, mayai, maziwa, samaki, maharage, n.k. Kwa kula vyakula hivi mwili utaweza kutibu majeraha kwa haraka zaidi.

2. Pumzika vya kutosha
Kupumzika ni njia ya kuupa mwili nafasi ya kujijenga na kujitibu wakati wa majeraha. Kutokana na mtindo wa maisha au changamoto za kiuchumi, baadhi ya watu hawapati muda wa kupumzika wapatapo majeraha.

Hivi leo utamkuta mtu akiendelea na shughuli zake huku akiwa na plasta, au bandeji bila hata kujali. Ili uweze kupona mapema unahitaji kuupumzisha mwili kwa kiasi cha kutosha ili upone vyema.

3. Fuata maelekezo
Kutokana na majeraha uliyoyapata daktari anaweza kukataza usile au sifanye kitu fulani lakini wewe hutaki; je unafikiri utaweza kupona mapema?

Watu wengi hukatazwa vitu kama vile pombe au kazi ngumu mara wapatapo majeraha, lakini ni wachache ndiyo wanaoheshimu hili.

Ni lazima ufuate ushauri wa daktari ikiwa unataka kupona mapema.

4. Kunywa maji mengi
Maji huchukua takriban asilimia 70 ya mwili wa binadamu. Kunywa maji mengi uwapo na majeraha kutakuwezesha kupona majeraha yako mapema.

Maji huboresha kinga mwili, huboresha misuli pamoja na viungio (joints) mbalimbali hivyo kukuwezesha kupona majeraha mapema.

5. Ogea maji ya baridi
Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa kuna manufaa makubwa ya kuogea maji ya baridi. Manufaa haya pia yapo kwa mtu aliyepata majeraha.

Kuogea maji ya baridi kutasababisha mzunguko mzuri wa damu, hivyo viini lishe na tiba vitasafirishwa vyema kwenda kuponya majeraha; pia maji baridi hupunguza maumivu ya vidonda au majeraha.

Kwa hakika lishe bora ni tiba ya maradhi takriban yote. Katika makala hii umeona jinsi lishe bora pamoja na kuzingatia kanuni chache za msingi za afya kunaweza kukusaidia kupona majeraha mapema

Vyakula 10 bora anavyotakiwa kula Mama mjamzito

Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na madini yote kama vitamini na protini. Mama mjamzito anatakiwa apate gramu 100 za protini kila siku. Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora.

Hivi ndivyo vyakula 10 bora ambavyo mama mjamzito na mtoto wake wanastahili kula;

1. Jamii Kunde 
Mbegu za kunde ni sehemu muhimu ya chakula kwa mama mjamzito kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini. Kwa watu wasiokula nyama au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama mbegu za jamii kunde zinatosheleza mahitaji ya protini. Hivi ni vyakula vya mimea kama Soya,Peas,Karanga, Alfa alfa,Mikunde, maharage.

2.Mayai 
Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protini, vitamini A na madini ambayo itasaidia kuzuia kupatwa na maradhi ya magonjwa mbali mbali.

3. Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa 
Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi na siagi. Maziwa ni muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa na misuli, Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mdundo wa moyo.

4. Viazi tamu 
Viazi vitamu vina vitamini A ambayo husaidia ukuaji wa macho ya mtoto,ngozi na mifupa

5. Nyama
Nyama ya kuku au ngombe huwa na protini nyingi sana na husaidia katika ukuaji wa mwili wa mtoto hasa kwa mama mjamzito wa miezi minne

6. Nafaka na vyakula vya Wanga 
Vyakula hivi huipa mwili nguvu ya kufanya kazi na pia ukuaji wa mtoto tumboni.Vyakula hivi ni kama mahindi,mtama ,mihogo,vyakula vya ngano kama mkate n.k.

 7. Avocado 
Ni matunda ambayo yana mafuta mengi maarufu kama fatty acid. Avocado inasaidia katika ukuaji wa ubongo,ngozi nyororo na ukuaji wa misuli ya mtoto tumboni.

8 .Mboga za majani 
Mboga za majani kama spinach, kabeji, mchicha na matembele. Mboga hizi zinafaa ziwe zenye rangi ya kijani iliyokolea kwa sababu hizi ndizo zenye virutubisho vya kutosha. Mboga hizi zitampa mama na mtoto wake Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kupata protini ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata ugonjwa wa Anemia.

9. Mafuta ya samaki 
Mafuta ya maini ya samaki huwa na Omega fatty acids ambayo inasaidia ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto.

10.Maji 
Maji ni muhimu kwa mwili kwa sababu inasaidia kwenye mmenyenyo na unyonywaji chakula na pia husaidia kuzia choo ngumu Maji pia huzuia uvimbe wa mwili na maambukizi ya mfumo wa mkojo(UTI)